Kikosi cha Yanga leo Jumamosi kitashuka kwenye uwanja wa CCM Kirumba kuikabili na Pamba Fc kwenye mchezo wa kirafiki ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Kubwa Kuliko Kanda ya Ziwa
Uongozi wa Yanga umelazimika kuiomba TFF iwaruhusu kumtumia mlinda lango Ramadhani Kabwili aliyekuwa timu ya Taifa ya vijana
Kabwili tayari ametua jijini Mwanza kwa ajili ya mchezo huo
Yanga inakabiliwa na changamoto ya golikipa baada ya walinda lango wake wote kuitwa timu za Taifa
Farouk Shikalo yuko Kenya na Harambee Stars, Metacha Mnata yuko na kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' na Kabwili aliitwa timu ya vijana U20
ADVERTISE HERE