Wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, Yanga wako mkoani Mwanza ambapo leo watashuka kwenye uwanja wa CCM Kirumba kumenyana na Pamba Fc
Mchezo huo ni sehemu ya maandalizi ya kikosi cha Mwinyi Zahera ambacho Jumamosi ijayo kitashuka uwanja wa Taifa kuikabili ZESCO United
Yanga ilitua Mwanza Jumatano iliyopita, imekuwa ikijifua kwenye uwanja wa CCM Kirumba
Zahera atakuwa na nafasi ya kujaribu silaha zake, msisitizo ukiwa zaidi kwenye safu ya ushambuliaji ambayo inasuasua
Yanga itawakosa nyota wake nane, sita wakiitwa timu za Taifa, wengine wakiwa na matatizo mbalimbali
Beki Paulo Godfrey ni majeruhi wakati Juma Abdul amefiwa na mama yake
Farouk Shikalo, Metacha Mnata, Mohammed Issa, Kelvin Yondani, Abdulaziz Makame na Patrick Sibomana wanakabiliwa na majukumu ya timu za Taifa