Yanga yaipa Toto Africans msaada wa jezi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Sep 2019
Yanga yaipa Toto Africans msaada wa jezi

Wakati Toto Africans ikijiandaa kushuka uwanjani kesho Jumanne kuwakabili Yanga katika mchezo wa kirafiki, viongozi wa Yanga tawi la Mwanza wameikabidhi timu hiyo jezi kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Daraja la pili.

Yanga itawavaa Toto 'Wanakishamapanda' kesho ikiwa ni mechi yake ya pili jiji Mwanza kujiweka tayari na mechi yake ya Ligi ya mabingwa Afrika itakayopigwa Jumamosi ya wiki hii dhidi ya Zesco.

Akikabidhi vifaa hivyo, Mwenyekiti wa matawi ya Yanga Mwanza, Saleh Akida amesema wameamua kuisapoti timu hiyo ili kuiwezesha kufanya vizuri katika Ligi yao.

"Thamani ya vifaa ni Sh 500,000 ikiwa ni jezi na soksi, lengo ni kuisapoti timu hii yenye historia kubwa nchini, wadau wengine wajitokeze kuipa nguvu, tumejipanga sisi Yanga Mwanza kupitia kampuni yetu ya Kabunda Security kutoa kile tulichonacho," alisema Akida.

Mwenyekiti wa Toto Africans, Rajabu Mbaramwezi alisema msaada huo ni muhimu kwao kwani awali walikuwa na pea moja, hivyo kwa sasa imeongezeka nyingine ambayo itawasaidia.

"Niwashukuru sana Yanga kwa msaada huu, hakika inatupa nguvu na kutambua tuko nao pamoja niombe tuendelee kushirikiana, lakini niwakaribishe wadau wengine kutusapoti" amesema Mbaramwezi"

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
10h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’