Dk Msolla aita mashabiki uwanja wa Taifa Jumamosi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Sep 2019
Dk Msolla aita mashabiki uwanja wa Taifa Jumamosi

Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa, uwanja wa Taifa, Jumamosi

Septemba 14 Yanga itashuka dimba hilo la Mkapa kuikabili Zesco United katika mchezo wa kwanza kusaka nafasi ya kutinga makundi

Dk Msolla amesema ameridhishwa na maandalizi ya timu jijini Mwanza, ana matumaini makubwa kuelekea mchezo wa Jumamosi

"Tunafanya maandalizi mazuri Mwanza, Mwalimu ameendelea kuwaweka vijana sawa kwa mchezo huo"

"Timu yetu iko vizuri, mashabiki waje kwa wingi Jumamosi waone Burudani," amesema

Aidha akizungumzia mwenendo wa timu hasa baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Pamba, Dk Msolla amesema kuna tofauti kati ya mechi ya mashindano na mechi ya kirafiki.

"Hii michezo ya kirafiki tunayocheza sio mashindano, ni sehemu ya mazoezi. Mwalimu anaitumia kujaribu mbinu na kurekebisha mapungufu yaliyopo"

"Lakini mechi za mashindano huwa tofauti"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’