Kibarua cha Lwandamina kipo salama - Sanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Oct 2017
Kibarua cha Lwandamina kipo salama - Sanga
Kaimu mwenyekiti wa Yannga, Clement Sanga amesisitiza kibarua cha Kocha George Lwandamina kipo salama kwa sasa.

Kocha Lwandamina amekuwa katika wakati mgumu kutoka kwa mashabiki wa Yanga wanaotaka atimuliwe kwa sababu ya mwenendo usiolidhisha wa mabingwa hao katika msimu huu, hasa baada ya suluhu dhidi ya Mtibwa Sugar mwishoni mwa wiki.

Akizungumza na MCL, Sanga ambaye pia anagombea nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi kwenye kampeni zinazoanza wiki ijayo alisema tumeona hizo taarifa, lakini kuna wengine wanayazungumza hayo niseme tu hatujawahi hata kukutana kufikiria kufanya mabadiliko wala kuhoji uwezo wa kocha wetu yoyote kwasasa sio tu huyo Lwandamina yoyote yule.

"Mimi ndiye kiongozi wa klabu nakuthibitishia hakuna uamuzi hayo nafikiri kuna watu wana mipango yao huko pembeni, lakini kwetu kama uongozi hatujafikiria kitu kama hicho bado tuna imani na makocha na hata timu yetu kwa ujumla.

Sanga ni kaimu Mwenyekiti wa Yanga kwasasa baada ya Yusufali Manji kujiuzulu alisisitiza kunawezekana kukawa na mapungufu kidogo ambayo kama uongozi tunayajua na tunayafanyia kazi ambayo hatuwezi kila kitu tukakiweka wazi lakini kama kuhusu hilo suala la kubadili kocha hatujafanya kikao cha kujadili kumleta kocha yoyote hapa pengine kuna Yanga nyingine ya tofauti huko lakini Yanga ninayoingoza mimi hatujawahi kufikiria kitu kama hicho.

"Yanga tuna historia tofauti na timu zingine ambazo zimekuwa hazikai na makocha,siku zote tumekuwa hatutaki kuingilia majukumu ya makocha tunataka kuona makocha wetu wanapata nafasi nzuri ya kufanya kazi zao.

"Tunaamini makocha waliona changamoto hizo na watazifanyia kazi nafikiri bado timu yetu watu wanatakiwa kukumbuka kuna baadhi ya wachezaji tunawakosa mpaka sasa kutokana na majeruhi mfano mtu kama Tambwe (Amissi) tunakumbuka kwamba takwimu zinaonyesha ndiye aliyekuwa mfungaji bora wetu namba mbili nyuma ya Msuva (Simon) ambaye ameondoka pia lakini Tambwe hajaweza kurudi ndiyo tunasikia ameanza mazoezi kwahiyo kuna mambo mengi kuhusu timu kutokufunga,"alisisitiza Sanga.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’