Zahera ampa Molinga mabao 20

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Sep 2019
Zahera ampa Molinga mabao 20

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera leo baada ya mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika uwanja wa Taifa, alipata nafasi ya kuzungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo dhidi ya ZESCO United

Pamoja na kuweka bayana maandalizi ya kikosi chake, Zahera alijibu maswali ya waandishi wa habari waliohoji kuhusu makali ya mshambuliaji wake David Molinga ambaye wengi wameonyesha kutokuwa na imani nae

Zahera amesisitiza kuwa Molinga atapata mafanikio Yanga, ni suala la muda tu

"Makambo ambaye mnamsifia hapa, kwenye ligi ya Congo alifunga mabao saba, Molinga amefunga mabao 15, sasa mniambie kati ya Makambo na Molinga nani aliyefunga mabao mengi Congo?," Zahera aliwauliza waandishi wa habari

"Nikwambie kama Molinga hakufunga mabao 15 au 20 kwenye ligi hapa Tanzania nitakupa dola 1000...!"

Kuelekea mchezo dhidi ya ZESCO Zahera amesema wamekamilisha maandalizi yao ambapo wameweza kupitia michezo mbalimbali ya ZESCO ambayo imewasaidia kufahamu ubora na udhaifu wa wapinzani wao

Hata hivyo Yanga itaikabili ZESCO United bila ya Molinga ambaye ataruhusiwa kuitumikia timu hiyo kama itafanikiwa kutinga hatua ya makundi

Usajili wa Mcongomani huyo ulifanyika nje ya muda uliokuwa umetolewa na CAF

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’