Kiungo Mapinduzi Balama amedhihirisha anaweza kuwa mbadala wa Paulo Godfrey katika nafasi ya ulinzi wa kulia
Jana Balama alicheza namba mbili kwa dakika 75 mechi dhidi ya ZESCO United
Katika michezo mitatu iliyopita, kocha Mwinyi Zahera amemtumia Balama nafasi hiyo kutokana na Boxer kuwa majeruhi
Balama alitolewa baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Ally Ally
Katika mchezo huo, Balama alionekana kutimiza vyema majukumu ya ulinzi na kufanya vizuri zaidi wakati timu inashambulia
Pamoja na kuwa Yanga ililazimishwa sare ya bao 1-1, yeye na wachezaji wengine walijituma kuipigania timu kuhakikisha inapata matokeo
ADVERTISE HERE