Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema wamejipanga kuhakikisha wanapata matokeo katika mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Zesco United nchini Zambia
Yanga itasafiri kuelekea Zambia kuwakabili mabingwa wa nchi hiyo, Zesco Septemba 28
Tayari kikosi cha Yanga kimeanza kujifua leo kuelekea mchezo huo
Aidha Dk Msolla amesema timu itakwenda mapema kuweka kambi nchini Zambia
"Timu itafanya maandalizi mazuri kuelekea mechi ya Marudiano ya Klabu Bingwa dhidi ya Zesco"
"Timu itaondoka nchini mwanzoni mwa wiki ijayo ili kuweka kambi Nchini Zambia kwa muda wa wiki nzima kabla ya kurejeana na Zesco, " Dk Msolla aliiambia eFM
Katika hatua nyingine Dk Msolla amewataka mashabiki wa Yanga wawe watulivu na kuwa na imani na kocha Mwinyi Zahera kwani anaamini ataipa mafanikio timu hiyo
DK Msolla amesema ni mapema sana kufikiria kufanya mabadiliko ya kocha kwa kuwa Mcongomani huyo ndio kwanza ameanza kuijenga timu