Kikosi cha timu ya Taifa kilichotangazwa leo, Jumapili ijayo Septemba 22 kitashuka dimba la Taifa kuikabili Sudan kwenye mchezo wa kusaka tiketi ya fainali za michuano ya CHAN kwa wachezaji wanaocheza ndani
Mchezo wa marudiano utapigwa Sudan Oktoba 18 2019
Ligi Kuu itasimama kupisha mchezo huo ulio ndani ya kalenda ya CAF
Yanga sasa imepata ahueni zaidi kwani mchezo dhidi ya Tanzania Prisons ambao ulikuwa upigwe Septemba 21 mkoani Mbeya hautakuwepo
Yanga itakuwa na muda wa kutosha kujiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Zesco United ambao utapigwa Zambia Septemba 28
Mabingwa hao wa kihistoria wameanza program maalum ya mazoezi ya Gym leo ambapo Kocha Mwinyi Zahera amesema watakuwa na ratiba ngumu ya mazoezi kabla ya kuifuata Zesco mwanzoni mwa wiki ijayo