Kama itafanikiwa kutinga hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa/Kombe la Shirikisho, Yanga itaweza kumtumia mshambuliaji wake mpya David Molinga
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Dismas Ten amesema ITC ya Molinga pamoja na beki Mustafa Suleyman walichelewa kuzipata hivyo hawakuwahi kuwaombea wachezaji hao leseni
Yanga inakabiliwa na changamoto kwenye safu yake ya ushambuliaji. Kama Molinga angepata leseni pengine angeongeza nguvu kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Zesco nchini Zambia
Hata hivyo bado uongozi wa Yanga haujakata tamaa kufuatilia leseni yake ambapo umemtuma mwakilishi kwenda jijini Cairo yalipo Makao Mkuu ya Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) kuona uwezekano kama mshambuliaji huyo anaweza kupatiwa leseni kama ilivyokuwa kwa mlinda lango Farouk Shikalo
Leseni ya Shikalo iliwasili siku chache kabla ya mchezo dhidi ya Zesco