Licha ya kocha wa Zesco United, George Lwandamina kutamba kuwa timu yake haijawahi kufungwa katika uwanja wake wa nyumbani tangu mwaka 2014, kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema watakuwa timu ya kwanza kushinda nchini Zambia
Akizungumza leo muda mfupi kabla ya kukwea pipa kuelekea Zambia, Zahera alisema wanahitaji kushinda kwa bao 1-0 tu ili waweze kutinga makundi
"Kule Zambia tunahitaji bao moja tu ili kuingia hatua ya makundi, hatuna shida ya kufunga mabao 100 tukipata moja tu litatutosha na kutuvusha hatua hii," alisema
Aidha Zahera amesema wamejiandaa kikamilifu wakiwa wamefanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza kwenye mchezo wa kwanza
Zahera aliondoka asubuhi ya leo akiwa na wachezaji 10 katika msafara wa kwanza wa timu hiyo
Wachezaji waliobaki pamoja na viongozi wengine wa benchi la ufundi wataondoka saa mbili usiku leo Jumanne