Malimi Busungu afunguka kilichomkwamisha Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Oct 2017
Malimi Busungu afunguka kilichomkwamisha Yanga
Mshambuliaji wa zamani wa Yanga ambaye sasa anafanya vizuri na klabu ya Lipuli FC Malimi Busungu amefungua kilichomkwamisha kun'gara kwenye kikosi cha Yanga.

Aliposajiliwa na Yanga kutoka Mgambo Shooting misimu mitatu iliyopita, Busungu alikuwa na uwezo mkubwa wa kupachika mabao.

Msimu mmoja kabla ya kutua Yanga alikuwa mmoja wa vinara wa upachikaji mabao katika ligi kuu ya Vodacom akiwa na Mgambo Shooting ya Tanga.

Haya ni mahojiano baina yake na mtandao wa ShaffihDauda;

Kwa nini hakupata nafasi ya kucheza akiwa Yanga?

Ni kweli nilipokuwa Yanga sikupata nafasi ya kucheza kama nilivyotarajia. Mwanzoni nilikuwa napata nafasi lakini baada ya kuondoka aliyekuwa kocha msaidizi Charles Boniface Mkwasa kwenda kuifundisha timu ya taifa kila kitu kikabadilika kuanzania hapo.

Kuondoka kwa Mkwasa ndani ya Yanga kulibadili kila kitu kwenye timu kwa upande wangu, nikawa sichezi na thamani yangu ikashuka kwenye kikosi.

Mambo yalilivyokuwa chini ya utawala wa Hans van Pluijm

Kuna mambo mengi sana juu ya hilo, siwezi kusema kila kitu kilichokuwa kinatokea lakini kuna watu wanajua ukweli wote. Kuna chuki zikaanza kupandikizwa na baadhi ya watu juu yangu kwa hiyo siwezi kuanza kutaja watu kwa majina lakini wao wanajijua.

Je ubora wa wachezaji wengine kwenye nafasi yake ulikuwa kikwazo kwake?

Sio kweli na siamini katika hilo, mimi najiamini ni mchezaji mzuri ndio maana waliamua kunisajili kwenye timu yao kuhusu suala la kushindwa kupata nafasi kwa sababu ya uwepo wa wachezaji fulani kwangu halipo, kwa sababu kuna wakati nilikuwa nacheza na kufanya vizuri.

Kutoonekana kwenye timu kwa muda mrefu

Lengo la kila mchezaji kwenye kila timu ni kupata nafasi ya kucheza na kuonekana, sasa kama huchezi na hupati nafasi maana yake nini? Unaishia kufanya mazoezi halafu hupangwi hata kwenye benchi la wachezaji wa akiba haupo inashusha morali yako kiuchezaji.

Kuna wakati kuna timu zilikuwa zinakuja zinataka kunisajili lakini kuna viongozi walikuwa wanakataa kuniruhusu niondoke ndio maana niliamua kukaa nikasubiri hadi mkataba wangu ulipomalizika nikaondoka. Sasa hivi nipo kwenye klabu ambayo naamini nitafanya vizuri kwa sababu mchezaji anaweza kufanikiwa popote ili mradi anaonesha uwezo wake haijalishi ni timu gani.

Ujio wa Lwandamina haukubalidili kitu

Kama nilivyosema mwanzo, nilikuwa sichezi sio kwa sababu sina uwezo kuna mambo mengi sana hapa, mengine sio poa kuyaanika hadharani nabaki nayo mimi mwenyee lakini kuna watu walikuwa wanapandikiza chuki ili mimi nisipate nafasi ya kucheza Yanga.

Kwa hiyo ujio wa kocha mpya haukubadili chochote kwa upande wangu, ndio maana niliendelea kubaki nje ya timu.

Malengo hayakutimia Yanga

Nikiwa Yanga malengo yangu hayakutimia, nilienda pale nikiwa na malengo ya kucheza na kuonekana lakini hilo halikuwezekana. Hayo ndio maisha ya mpira unaweza ukashindwa kutimiza malengo sehemu lakini yakatimia ukiwa sehemu nyingine ndio maana nipo Lipuli ambako nina amani na nadhani nipo sehemu sahihi kwa ajili ya kutimiza kile kilichoshindikana semu nyingine.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
5h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’