Uwaja wa Levy Mwanawasa ulizinduliwa mwaka 2012, ukiwa umejengwa kwa msaada wa Jamhuri ya watu wa China
Uwanja huo una uwezo wa kuchukua mashabiki 49,000/- ukiwa ni pungufu ya mashabiki 11,000 kuweza kufikia uwanja wa Taifa
Umejengwa katika Mji wa Ndola, ni wa nyasi asili, mazingira ambayo Yanga imekuwa ikikutana nayo kwenye uwanja wa Taifa
Jina la Levy Mwanawasa lilibadilishwa na aliyekuwa Rais wa Zambia Michael Sata ikiwa ni heshima kwa rais wa tatu wa Taifa hilo
Awali uwanja huo ulikuwa ukiitwa Ndola

Jumamosi Septemba 28 Yanga itashuka dimbani hapo kusaka ushindi muhimu utakaowapa nafasi ya kutinga hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa
Yanga ina faida ya kucheza katika uwanja huo kwani mazingira yake yanafanana kabisa na yale ya uwanja wa Mkapa
Hakika, Jumamosi patachimbika hapo Ndola