Yanga 'yatia maguu' kwa Miquissone

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Oct 2019
Yanga 'yatia maguu' kwa Miquissone

Unamkumbuka yuke mshambuliaji wa UD Songo aliyewafunga Simba walipokuja kucheza jijini Dar es salaam?

Anaitwa Luís Miquisson, taarifa zinaeleza yuko kwenye rada za Yanga

Baada ya safu ya ushambuliaji ya Yanga kuanza kwa kusuasua, imeelezwa mchakato wa kusaka washambuliaji ili kuiongezea nguvu safu hiyo umeanza

Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindi Msolla ameeleza kuvutiwa na mshambuliaji huyo na amekiri kutuma watu wamfuatilie

"Wachezaji tulionao si wabaya sana, tatizo tulilonalo tumeingiza wachezaji wengi wapya, wanahitaji muda wa kukaa pamoja kwa muda mrefu…kwanza hata kwa timu ilivyo sasa, mwalimu Zahera (Mwinyi), amejitahidi sana," Dk Msolla amenukuliwa na gazeti la Bingwa

"Pamoja na hilo, tunahitaji kupata wachezaji wa kiwango cha juu zaidi wa kuamua matokeo…mchezaji kama yule wa UD Songo (Miquissone) ambaye shughuli yake sote tuliiona walipocheza na Simba. Ukiwa na wachezaji wawili au watatu kama wale, unakuwa na uhakika wa ushindi."

Alipoulizwa iwapo Miquissone yupo katika mipango ya Yanga, Dk. Msolla alisema:

"Ndiyo, kuna mtu analishughulikia hilo, lakini pia tunaendelea kuwafuatilia wengine wenye kiwango cha juu kutoka katika timu hizi zilizopo Ligi ya Mabingwa, tutaangalia wale watakaong’ara hatua za awali na raundi ya kwanza kabla ya kuingia makundi"

Pamoja na Luis, Yanga pia huenda ikajaribu kumuwania mshambuliaji wa Platinum FC Perfect Chikwende ambaye juzi aliiangamiza UD Songo kwa kufunga hat-trik kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa na kuipeleka timu hiyo hatua ya makundi

Hata hivyo Yanga haitaweza kumpata mchezaji huyo wakati huu labda mpaka mwezi Juni wakati wa dirisha kubwa la usajili

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
11h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
15h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
16h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
16h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’