Zahera ataja sababu ya kutomtumia Abdul

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Oct 2019
Zahera ataja sababu ya kutomtumia Abdul

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema hana tatizo na beki wa kulia wa timu hiyo Juma Abdul na anafahamu ni mchezaji mzuri lakini amesisitiza ni lazima awe 'fit' kuweza kwendana na kasi anayotaka

Kumekuwa wa presha kubwa kutoka kwa mashabiki ambao wamekuwa wakihoji sababu ya Abdul kutocheza kwenye kikosi cha kwanza huku Zahera akiwatumia baadhi ya wachezaji katika nafasi wasizostahili

Mfano beki ya kulia anapokosekana Paulo Godfrey 'Boxer', amekuwa akiwatumia Ally Ally, Mustafa Suleyman, Mapinduzi Balama na Cleofas Sosopeter badala ya Abdul ambaye miaka yote amekuwa akicheza nafasi hiyo

Aidha Zahera amewataka mashabiki wawe watulivu na kuacha kuingia majukumu ya kiufundi

"Unajuwa mashabiki wao wanataka kuwa makocha wapange wao kikosi. Mimi ndiye ninayekaa na wachezaji muda mwingi hivyo nafahamu nani ni bora zaidi ya mwingine"

"Juma msimu uliopita hajacheza michezo mingi wachezaji ninaowapa nafasi wamecheza wakiwa katika timu zao," amesema

"Sina maana kwamba ni mchezaji mbaya hapana ni mzuri na amekuwa akipambana kusaka nafasi ya kucheza muda ukifika atapata nafasi hiyo kwa sasa naomba majukumu yangu niachiwe mwenyewe nisiingiliwe,"

"Mpira wa Tanzania unaendeshwa na mashabiki wao wakipata matokeo wanasahau kabisa kuwa waliocheza ni wachezaji wasiowapenda wakikosa matokeo pia hawakosi kitu cha kuzungumza"

Abdul alikuwa sehemu ya kikosi kilichosafiri Zambia wiki iliyopita ambapo mwishoni mwa wiki kilicheza na Zesco United mchezo wa ligi ya mabingwa na kupoteza kwa kufungwa mabao 2-1

Zahera alimtumia Ally Ally beki ya kulia huku Abdul akiwa miongoni mwa wachezaji waliokuwa benchi

Pengine beki huyo anaweza kupata nafasi ya kucheza kwenye michezo ya ligi kuu ya Vodacom ambayo Yanga itacheza wiki hii

Alhamisi Yanga itacheza na Polisi Tanzania uwanja wa Uhuru kisha kurejea dimbani hapo siku ya Jumapili kuikabili Coastal Union

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’