Zimiseleni Moyo anakaribia kutua Jangwani

Admin By Admin
β€’
30 Jun 2017
Zimiseleni Moyo anakaribia kutua Jangwani
Zimiseleni Moyo ni kiungo mkabaji kutoka Zimbabwe ambaye anakipiga na klabu ya Zanaco, mabingwa Zambia.

Huyu jamaa anatumia zaidi mguu wa kushoto, ni mchezaji anayeweza kucheza nafasi nyingi dimbani

Kwa aliyefuatilia michezo ya miwili ya Yanga dhidi ya Zanaco kwenye michuano ya ligi ya mabingwa ni dhahiri atakuwa amefahamu mchezaji ninaemzungumzia hapa.

Huyu jamaa yuko kwenye timu ya Taifa ya Zimbabwe na huenda kocha George Lwandamina akafanikisha jembe hili kutua Jangwani kumaliza kabisa wasiwasi kwenye nafasi ya kiungo mkabaji.

Katika ligi kuu ya Zambia hadi sasa Moyo ameweka rekodi ya kuwa kiungo aliyetoa pasi nyingi zilizofika kwa walengwa kuliko wengine, lakini pia ana rekodi ya kiungo aliyetibua zaidi mipango ya wapinzani kuliko mwingine kwenye ligi ya Zambia.

Ukizungumzia 'mkata umeme' basi huyu ndiye mwenyewe sio yule aliyenunuliwa msimu uliopita, Justine Zulu.

Moyo anafahamiana vizuri na Thabani Kamusoko ambaye walicheza pamoja nchini Zimbabwe katika timu ya Highlanders.

Mwenyewe amefunguka kuwa amevutiwa na klabu ya Yanga na hatasita kujiunga kama kila kitu kitakwenda sawa.

Yanga imedhamiria kukamilisha usajili wake kwa kuwa anafiti kabisa mapendekezo ya kocha kupata mchezaji wa kiungo wa kushoto atakeyeweza kucheza zaidi ya nafasi moja.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’