Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kuwa ukarabati wa uwanja wa Kaunda unaendelea ambapo mkapa kufikia February 2020 utakuwa umekamilika
Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema zoezi la kujaza kifusi limekamilika, kazi inayofanyika sasa ni usambazaji wa kifusi hicho tayari kuanza zoezi la kupanda nyasi
"Tunaendelea na ujenzi wa uwanja wetu wa Kaunda ambao hivi sasa upo kwenye hatua ya kusawazazishiwa udongo, kuna greda mbili ambazo zinafanya kazi hiyo," amesema
"Baada ya kusawazisha udongo huo, zoezi litakalofuata ni kuweka udongo mwingine ambao ni wa rutuba kisha upandaji wa nyasi utafuatia, na mpaka kufikia raundi ya pili ya ligi unaweza kuwa umekamilika"
Hivi karibuni Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Dismas Ten alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa, kutokana na ukubwa wa eneo hilo, watatoa viwanja viwili, kimoja cha nyasi bandia na kingine cha nyasi asili
Kuhusu ujenzi wa uwanja wa Kigamboni, Mwakalebela amesema mchakato inaendelea ambapo kuna Kamati maalum imeundwa kusimamia zoezi la hilo
Jana Yanga iliweka hadharani wajumbe wa Kamati hiyo inayosimamia masuala yote ya ujenzi na Miundombinu
Kukamilika kwa uwanja wa Kaunda kutaipunguzia timu hiyo gharama za kukodi viwanja
Yanga imekuwa ikifanya mazoezi uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini jijini Dar es salaam