Kiungo Issa Bigirimana amerejea rasmi kikosini baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yakimsumbua
Bigirimana amejumuishwa kwenye kikosi cha Yanga kilichojichimbia kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya Polisi Tanzania ambao utapigwa kesho Alhamisi kwenye uwanja wa Uhuru
Kiungo huyo mwenye kasi ya kimbunga, amekosekana kwenye kikosi cha Yanga kwa muda mrefu akiuguza majeraha aliyopata mkoani Morogoro wakati wa maandalizi ya msimu mpya
Amesema baada ya kupona jukumu lake la kwanza ni kuhakikisha anaisaidia Yanga kupata ushindi katika michezo yake
ADVERTISE HERE