Kilichoiponza Yanga leo ni hiki

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
3 Oct 2019
Kilichoiponza Yanga leo ni hiki

Yanga iliuanza mchezo wa leo dhidi ya Polisi Tanzania kwa kasi kubwa, wachezaji wakionekana kuwa na shauku ya kupata matokeo

Iliwachukua dakika sita tu kufunga bao la kuongoza kupitia kwa Mrisho Ngasa

Lakini baada ya kufunga bao hilo wachezaji walipunguza kasi, hali hiyo ilitoa nafasi kwa Polisi Tanzania kuuchukua mchezo

Mara kwa mara Yanga imekuwa ikikumbwa na changamoto hii ya wachezaji kuridhika baada ya kufunga bao la kuongoza

Mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa dhidi ya Zesco uliopigwa uwanja wa Taifa, hali ilikuwa hivyohivyo

Yanga imekuwa timu inayocheza kwa vipindi. Inacheza vizuri wakati inasaka bao, ikifunga wachezaji wana 'relax'. Watazinduka tena pale wanaporuhusu bao

Kama juhudi hizo zingekuwa zinawekwa kwa muda wote wa mchezo, Yanga ingekuwa inashinda ushindi mnono

Ni suala ambalo pengine benchi la ufundi linapaswa kukaa na wachezaji watambue ushindi haupatikani kwa kufunga bao moja

Yanga leo ilikuwa na uwezo wa kushinda mchezo kwa mabao mengi kama moto walioanza nao wangeuendeleza kwa muda mrefu zaidi

Kama wafanyavyo siku zote, wachezaji walikuja kuzinduka tena baada ya timu kuwa imeruhusu mabao mawili

David Molinga alidhihirisha ubora wake kwa kutumia nafasi mbili muhimu kuirejesha Yanga mchezoni

Uchovu wa safari umechangia

Kama ilivyokuwa mchezo wa kwanza dhidi ya Ruvu Shooting, wachezaji wa Yanga waliwasili kutoka Zambia juzi usiku, hivyo wamepumzika siku moja na leo kurejea dimbani

Sadney Urikhob alionekana dhahiri amechoka pamoja na Juma Balinya

Benchi la ufundi walifanya uamuzi sahihi wa kuwatoa wakati wa mapumziko

Mabao mawili yaliyofungwa na Nchimbi kwenye kipindi cha pili yalitokana na uzembe wa mabeki. Mtoni, Yondani na Lamine walipoteza umakini kwenye mchezo wa leo

Kwa kiasi flani,walionekana hawako kwenye ubora wao wa siku zote

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
10h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
14h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
15h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
15h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’