Mshambuliaji David Molinga leo amefunga mabao mawili muhimu ambao yameinusuru Yanga na kipigo kutoka Polisi Tanzania kwenye uwanja wa Uhuru
Mabao yake yameisaidia Yanga kutoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya Polisi Tanzania
Molinga alikumbana na ukosoaji mkubwa kutoka kwa mashabiki wengi waliokosa imani kutokana na umbile lake
Hata hivyo, ameanza kudhihirisha kuwa yeye ni mshambuliaji mwenye urafiki na nyavu
Amelidhihirisha hilo leo kwa kufunga mabao muhimu
Katika michezo mitatu iliyopita, Molinga amefunga mabao matano. Hizo sio takwimu za mshambuliaji wa kawaida
ADVERTISE HERE