Mapema leo Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu jijini Dar es Salaam ilimuachia huru Mfanyabiashara Yusuf Manji aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya matumizi ya dawa za kulevya.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu, Cyprian Mkeha alisema mahakama hiyo imefikia uamuzi huo baada ya upande wa mashtaka kushindwa kutoa ushahidi wa kujitosheleza hivyo mahakama hiyo kushindwa kuthibitisha iwapo Manji anatumia madawa ya kulevya.
Mkeha alieleza kuwa mahakama imejiridhisha kuwa mtuhumiwa alikuwa bado anatumia dawa mbalimbali kwa matibabu yake kulingana na maagizo ya daktari na dawa hizo zina vimelea vya morphine ambayo pia inaweza kukutwa kwenye heroine, kwa hiyo maabara ya Mkemia Mkuu ingeenda mbele zaidi kujua morphine iliyokutwa kwa mtuhumiwa imetokana na nini?
Manji alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Februari 16, 2017 akituhumiwa kwamba, kati ya Februari 6 na 9, 2017 katika eneo la Upanga Sea View, Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya heroine.
Manji ambaye alikuwa mshtakiwa alikuwa na mshahidi 7 wakati upande wa mashtaka ulikuwa na mshahidi watatu.
Hivi karibuni Manji pia aliachiwa huru katika kesi nyingine ya Uhujumu uchumi baada ya Jamhuri kuamua kutoendelea na kesi hiyo.

ADVERTISE HERE