Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amewataka Wanayanga kupuuza taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikiwa na lengo la kutengeneza migogoro
Dk Msolla amesema pamoja na changamoto za kiuchumi zinazoikabili Yanga, msimu huu wamejipanga na wanahakikisha wachezaji wanapata stahili zao kwa wakati
"Timu inahudumiwa vizuri, wachezaji wanapata mishahara yao kwa wakati na pia tumeanzisha utaratibu wa kuwapa posho kila wiki Tsh 100,000/- kwa mara ya kwanza kwani jambo hili halikuwahi kuwepo," amesema
"Tusikubali kuyumbishwa na watu wachache wanaoutumia mitandao ya kijamii kutaka kutuvuruga. Mimi kama Mwenyekiti nimekuwa mstari wa mbele kuvunja makundi baada ya uchaguzi"
"Ukiangalia hata Kamati ninazounda najitahidi kuwahusisha wadau wote kutoka makundi yote yaliyoshiriki uchaguzi"
"Najua kuna wachache ambao walikuwa wakinufaika na Yanga hapo awali wangependa kuona hatufanikiwi"
"Yanga ni timu yetu, tuwe wamoja ili tuhakikishe timu inafikia malengo tuliyojiwekea msimu huu"
Kutopata matokeo michezo ya hivi karibuni kulipelekea kuibuka kwa taarifa za mivutano baina ya viongozi huku taarifa nyingine zikidai wachezaji hawalipwi mishahara na posho zao kwa wakati jambo ambalo Dk Msolla amelipinga