Uongozi wa klabu ya Yanga umefafanua kutoonekana kikosini kwa Maneja wa timu hiyo Nadir Haroub 'Cannavaro' ambaye kwa sasa ni Meneja wa timu ya Taifa ya Tanzania
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema Mkataba wa Nadir na Yanga ulimalizika kabla hajaanza majukumu ya timu ya Taifa
Aidha Bumbuli amesema TFF iliwasiliana na Yanga baada ya kumteua nahodha huyo wa zamani wa mabinga hao wa kihistoria na walimtakia kila la kheri kwenye majukumu yake mapya
"Alivyokuwa Yanga TFF walitueleza kuwa wanamuhitaji, wakaambiwa mkataba wake umekwisha wanaweza kumtumia. Hata kama angekuwa na mkataba tungemruhusu aende kujiunga na benchi la ufundi la timu ya taifa huku atoe nafasi kwa watu wengine," amesema
"Tulimtakia kila la kheri kwani alikuwa mchezaji wetu tena nahodha na baadae Meneja"
Cannavaro alikuwa Meneja wa Yanga msimu uliopita akikabidhiwa majukumu hayo baada ya kustaafu soka
Ndiye mchezaji aliyeitumikia Yanga kwa muda mrefu zaidi katika historia ya klabu hiyo
Cannavaro amecheza Yanga kwa miaka 12 akivunja rekodi ya Fredy Mbuna aliyedumua Yanga kwa miaka 11