Kwa mara nyingine Yanga imerejeshwa nchini Misri safari hii ikipangwa na Pyramids Fc mchezo wa mtoano kusaka tiketi ya kutinga makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika
Habari njema ni kuwa Yanga haina historia ya 'kuboronga' inapokwenda kucheza Misri
Al Ahly na Zamalek, wanaifahamu vizuri shughuli ya Yanga kwani timu hizo zimecheza na Yanga mechi kadhaa huko kwao
Jambo pekee ambalo linawafanya Wamisri wafanikiwe wanapocheza kwao ni hujuma wanazofanya nje na ndani ya uwanja
Hivyo ili kuwa na nafasi nzuri ya kusonga mbele Yanga lazima ipate ushindi mnono nyumbani
Kikosi hiki cha kocha Mwinyi Zahera kimeonyesha uimara kinapocheza ugenini, kazi iliyobaki ni kuhakikisha kinapata matokeo nyumbani
Uongozi wa Yanga unapaswa kufanya kampeni kubwa kama ile ya wiki ya Mwananchi ili kuhakikisha Oktoba 27 uwanja wa Taifa unafurika mashabiki kuhakikisha Mwarabu anafungwa
Tena ikiwezekana muda wa mchezo uwe saa tisa Alasiri kwani Yanga itakapokwenda Misri itacheza saa nne au tano usiku wakati wa baridi kali