Beki wa kulia wa Yanga Paul Godfrey 'Boxer' amerejea kikosini baada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje kwa wiki tatu
Boxer ameanza mazoezi mepesi ambayo yatamuweka sawa kabla ya kuanza majukumu ya kikosi cha kwanza
Beki huyo kinda ameungana na Raphael Daudi na Issa Bigirimana ambao pia walikuwa nje wakiuguza majeraha
Yanga ilirejea mazoezini jana baada ya mapumziko ya siku tatu
Mabingwa hao wa kihistoria wanakabiliwa na mchezo wa ligi kuu Oktoba 22 mkoani Mwanza dhidi ya Alliance Fc
Aidha mchezo dhidi ya Mbao Fc ambao ulipangwa kupigwa Oktoba 26 ni dhahiri utasogezwa mbele kwa kuwa Oktoba 27 Yanga inakabiliwa na mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids Fc
ADVERTISE HERE