Dante anaikosea Yanga - Nugaz

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Oct 2019
Dante anaikosea Yanga - Nugaz

Uongozi wa klabu ya Yanga umemshukia beki wake Andrew Vicent 'Dante' ambaye amekataa kurejea kambini akishinikiza alipwe fedha anazoidai klabu hiyo

Msemaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema pamoja na uongozi wa timu hiyo kuwa tayari kumlipa kwa awamu fedha anazodai zinazofikia Tsh Milioni 40, beki huyo amegoma kurejea kikosini

"Yanga tulikuwa tayari kumlipa kwa awamu tatu, Mil 15 mara mbili kisha kumalizia Mil 10"

"Yeye si mchezaji pekee anayeidai Yanga, wengine tumefanya nao makubaliano ya aina hiyo, wamekubali"

"Lakini Dante anaikosea Yanga kwa kuwa ameendelea kupokea mshahara bila ya kufanya kazi"

"Madai yake alipaswa kuyafanya huku akiwa kazini. Huo ndio utaratibu wa kazi mahali popote"

"Yeye kama hataki mpaka alipwe fedha zake kwa nini anaendelea kupokea mshahara wakati anajua hafanyi kazi?"

"Tayari wapo wanaohoji hatua hiyo kuwa pengine kuna mpango umejificha kama ule wa Beno, pengine dirisha dogo anataka kujiunga na timu nyingine. Sisi viongozi tunayajua ya ndani tu lakini ya huko nje nyie mashabiki mtakuwa mnayafahamu zaidi," alisema Nugaz

Dante amegoma kujiunga kikosi Yanga akishinikiza alipwe huku Juma Abdul ambaye alikuwa na madai, amekubali kurejea kikosini na anapokea malipo yake kwa awamu

Beki huyo kisiki hakujiunga kabisa na Yanga msimu huu akianza kwa kukosa maandalizi ya mwanzo wa msimu yaliyofanyika mkoani Morogoro

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
1h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
4h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
9h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
9h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
13h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’