Nyota wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania, Amri Kiemba amesema njia pekee ya Yanga kutinga hatua ya makundi michuano ya kombe la Shirikisho, ni kuhakikisha wanapata ushindi mnono nyumbani
Oktoba 27 Yanga itashuka dimba la CCM Kirumba kumenyana na Pyramids Fc kutoka Misri ukiwa ni mchezo wa raundi ya kwanza kusaka nafasi ya kutinga hatua ya makundi
Kiemba amesema mara nyingi timu za Tanzania huwa zinapata matokeo dhidi ya timu za Kaskazini katika michezo inayopigwa nyumbani lakini matokeo hayo mebamba huwa hayazisaidii kwenye michezo ya ugenin
Aidha Kiemba amesema licha ya Pyramids Fc kuwa timu isikuwa na uzoefu wa michuano ya CAF hii ikiwa mara yao yakwanza kushiriki, bado itakuwa timu hatari kwa Yanga kutokana na uwekezaji mkubwa wa timu hiyo na ubora wa ligi yao
"Naiangalia mechi hiyo kwa namna nyingine.Β Kwa tofauti ya ligi ya Tanzania na Misri naona bado ni timu ngumu haijalishi tunacheza na timu gani. Tusiangalie historia ya timu tu, tuangalie pia historia ya ligi wanayocheza. Mechi haitakuwa rahisi," amesema
"Mara nyingi timu za Tanzania zimekuwa na uwezo wa kupata matokeo hata kwa timu za Afrika ya Kaskazini (kwenye mechi za nyumbani) shida imekuwa mechi inapokuwa ugenini."
"Tumeshindwa pia kupata magoli ya kutosha hapa nyumbani ili yazisaidie timu zetu ugenini. Ukishinda goli 1-0 nyumbani kwa timu za Kaskazini mwa Afrika unakuwa kama tayari umeshatoka."