Mchezo wa ligi kuu ya Vodacom kati ya Mbao Fc dhidi ya Yanga ambao awali ulipangwa kupigwa Oktoba 24, sasa utapigwa Jumanne Oktoba 22 kwenye uwanja wa CCM Kirumba
Aidha mechi dhidi ya Alliance Fc ambayo awali ilipangwa kupigwa Oktoba 20, imesogezwa mbele
Uongozi wa Yanga umethibitisha kuwa mchezo dhidi ya Mbao umerudishwa nyuma ili kutoa nafasi kwa wawakilishi hao wa Tanzania Bara kujiandaa na mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids FC ambao utapigwa Oktoba 27 hapo CCM Kirumba
Yanga inatarajiwa kuondoka jijini Dar es salaam kuelekea Mwanza Oktoba 20
ADVERTISE HERE