Mechi ya kirafiki kati ya Yanga dhidi ya Pan African inapigwa kwenye uwanja wa Uhuru kuanzia saa kumi kamili jioni
Mchezo huo wa kujipima nguvu ni wa mwisho kabla ya kikosi cha Yanga kuelekea jijini Mwanza kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu na kombe la Shirikisho
Uongozi wa Yanga umewataka mashabiki wake wajitokeze kwa wingi uwanja wa Uhuru kuiunga mkono timu yao
Viingilio vya mchezo huo vimefanywa rafiki ili kuwarahisishia mashabiki kuushuhudia mchezo huo
VIP ni Tsh 5,000/- wakati Mzunguuko ni Tsh 2,000/-
Hii ni nafasi kwa mashabiki wa Yanga kushuhudia maendeleo ya kikosi chao kabla ya mechi muhimu mkoani Mwanza
Pan African sio timu ya kubeza, ni moja ya timu ngumu kutoka ligi daraja la kwanza
ADVERTISE HERE