Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatarajiwa kutangaza ajira ya Mtendaji Mkuu mpya wa Bodi ya Ligi baada ya kumbadilishia majukumu Boniface Wambura aliyekuwa Mtendaji wa Bodi hiyo
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF leo, Wambura hataongezewa mkataba, atarudishwa TFF kuwa Mkuu wa idara ya Habari na Masoko akisaidiwa na Cliford Ndimbo katika upande wa Habari kama Afisa Mkuu wa kitengo hicho pamoja na Aaron Nyanda kama Afisa Mkuu wa kitengo cha masoko.
Pia TFF imemtangaza Oscar Mirambo kuwa Mkurugenzi mpya wa ufundi wa shirikisho hilo
Mirambo ambaye aliwahi kuwa kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania U17 (Serengeti Boys) anachukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Ammy Ninje
ADVERTISE HERE