Kuelekea mchezo dhidi ya Pyramids Fc, Yanga bado haina uhakika na huduma ya beki wake kisiki Kelvin Yondani ambaye alipata majeraha kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union
Yondani hakusafiri na kikosi cha timu ya Taifa nchini Sudan kutokana na majeraha hayo
Zikiwa zimebaki siku 10 kabla ya mchezo huo utakaopigwa uwanja wa CCM Kirumba Oktoba 27, uongozi wa Yanga unahaha kuhakikisha beki huyo anapona kwa wakati
Kwani kukosekana kwake kunaweza kuwa pigo kwa Yanga ambayo pia itamkosa pacha wake Lamine Moro anayetumikia adhabu ya kadi mbili za njano
Lamine alipewa kadi nyekundu kwenye mchezo dhidi ya Zesco nchini Zambia baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano
Kwa sasa benchi la ufundi chini ya kocha msaidizi Noel Mwandila wanaonekana kuwaandaa Ally Mtoni na Mustafa Suleyman kuchukua nafasi za walinzi hao
Mtoni amekuwa akitumika nafasi ya ulinzi wa kushoto atalazimika kuingia kati wakati Marcelo/Jaffar wakitarajiwa kuchukua majukumu upande wa beki wa kushoto