Tambwe kupangua safu ya ushambuliaji ya Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
9 Oct 2017
Tambwe kupangua safu ya ushambuliaji ya Yanga
Mshambuliaji Amissi Tambwe, amerejea kwa kishindo klabuni hapo na anatarajiwa kupangua kikosi cha kwanza cha kocha George Lwandamina.

Tambwe tayari ameifungia timu hiyo mabao 46 ya Ligi Kuu Bara tangu alipojiunga nayo mwishoni mwa 2014. Nyota huyo raia wa Burundi yupo fiti baada ya kuwa nje ya Uwanja kwa kwa miezi miwili.

Kurejea kwa Tambwe aliyekuwa majeruhi, kunatarajiwa kuwatikisa washambuliaji wengine klabuni hapo akina Ibrahim Ajibu, Donald Ngoma na Obrey Chirwa ambapo mmoja atalazimika kumpisha katika kikosi cha kwanza.

Awali, Tambwe alifanya vizuri pindi akicheza sambamba na Ngoma ambapo msimu wa 2015/16 kwa pamoja walifunga mabao 38 ya ligi na kuwa pacha kali zaidi ya ushambuliaji katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja.

Hata hivyo uwepo wa Ajibu huenda ukapangua pacha hiyo kwa Lwandamina kumpanga na Tambwe ama kuwatumia watatu pamoja na Ngoma kwenye mchezo unaofuata dhidi ya Kagera Sugar.

Nyota wa zamani wa Yanga, Aaron Nyanda, amefichua kuwa Tambwe hana mpinzani katika kikosi cha kwanza na huenda kocha Lwandamina akalazimika kumpunguza kiungo mmoja ama mshambuliaji mmoja kumpisha.

“Tambwe lazima aanze na Ngoma (Donald) katika kikosi cha kwanza. Ajibu (Ibrahim) anaweza kuanza katika winga moja na kocha atabaki na maamuzi ya kuangalia nani kati ya Pius Buswita na Obrey Chirwa anastahili kuanza,” alisema Nyanda.

Yanga imekuwa na ukame wa mabao msimu huu na katika mechi tano za mwanzo imefunga manne tu, lakini Lwandamina anaamini kurejea kwa Tambwe kunaweza kuongeza kasi yao ya ufungaji.

Nyota mwingine wa zamani wa Yanga, Ali Yusuph ‘Tigana’ alisema Tambwe na Ngoma walifanya vizuri pamoja, lakini sasa kocha Lwandamina anaweza kujaribu kombinesheni mpya ya Tambwe na Ajibu.

“Bado Ngoma hajawa vizuri sana tangu alipotoka benchi la majeruhi, nimemuona Ajibu yuko vizuri, pengine kocha anaweza kumjaribu na Tambwe,” alisema Tigana.

Kwa hisani ya Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
4h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
9h ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
13h ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
14h ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
14h ago
READ MORE →
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
14h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
18h ago
READ MORE →
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE →
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →