Yanga yasaka ushindi muhimu dhidi ya Mbao Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Oct 2019
Yanga yasaka ushindi muhimu dhidi ya Mbao Fc

Kikosi cha Yanga kiko mkoani Mwanza ambapo leo jioni watashuka kwenye uwanja wa CCM Kirumba kuikabili Mbao Fc ukiwa ni mchezo wa ligi kuu ya Vodacom

Yanga mabingwa mara 27 ligi kuu ya Tanzania Bara watakuwa na kazi moja tu ya kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mchezo huo

Hata hivyo Mbao Fc imekuwa na kawaida ya kuwapa wakati mgumu vijana hao wa Jangwani hasa wanapokutana dimba la CCM Kirumba

Msimu uliopita kwa mara ya kwanza Yanga iliweza kupata ushindi dhidi ya Mbao hapo Kirumba baada ya kupoteza michezo mitatu kabla

Morali ya wachezaji wa Yanga iko juu hasa ikizingatiwa wanakabiliwa na mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids Fc Jumapili ya Oktoba 27

Matokeo ya ushindi yatawaweka katika nafasi nzuri ya kufanya vizuri mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na wakazi wa jiji la Mwanza na mikoa ya jirani

Jana jioni Yanga ilifanya maandalizi yake ya mwisho kwenye uwanja wa CCM Kirumba kuelekea mchezo huo

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera alisema vijana wake wako tayari kwa mchezo huo

"Kwa kawaida naiandaa timu kwa ajili ya mchezo uliokuwa mbele yangu, hadi sasa timu iko vizuri na tayari kwa mchezo dhidi ya Mbao FC"

"Tunawaheshimu Mbao ni timu nzuri, lakini na sisi ni wazuri pia na tumejiandaa kwa ushindi," alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’