Zahera ataja kinachoisumbua Yanga, timu za Tanzania

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Oct 2019
Zahera ataja kinachoisumbua Yanga, timu za Tanzania

Changamoto kubwa ambayo imekuwa ikimsumbua Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera tangu msimu uliopita, ni safu ya ushambuliaji katika kupachika mabao na kutumia nafasi zinazotengenezwa kwa usahihi.

Jambo hili amesikika mara kwa mara akilizungumzia na kusema kuwa kikosi chake hakina wachezaji wanaoweza kutengeneza shambulizi kali la kushtukiza (counter attack) kutokana na kukosa watu wanaoweza kutimua mbio kisawa sawa.

Mbali ya hilo, Zahera anaamini kwamba changamoto nyingine ndani ya kikosi chake ni wachezaji kutojua majukumu yao, ikiwamo usahihi wa kuomba pasi, kutoa pasi, kutengeneza nafasi, kufunga, kukaba na nidhamu kwa ujumla.

Mkongomani huyo alitoa kauli hiyo juzi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya kikosi chake kwa ajili ya kuivaa Mbao FC leo kwenye Uwanja wa CCM kirumba, Mwanza.

Zahera alisema kwamba tatizo hilo siyo kwa Yanga peke yake, bali ameliona kwa timu nyingi za Ligi Kuu Bara tangu alipotua nchini kukinoa kikosi cha Wanajangwani hao, jambo ambalo linasababisha vikosi vingi kutokuwa na ubora wa muendelezo.

Kutokana na changamoto hiyo, ndiyo maana kwenye mazoezi ya kikosi chake kila mara amekuwa karibu na wachezaji wake kuwakumbusha majukumu yao, ikiwamo kupiga pasi kwa usahihi na kuomba mpira kwenye eneo zuri na kutojisahahu kana kwamba watakuwa wanacheza peke yao uwanjani.

"Nafurahia kucheza jinsi tunavyotaka kucheza… mchezaji anaweza kuwaza kwamba vile anavyofanya ni vizuri, lakini hapana, hata vile Molinga (David) namna anaomba mpira, siyo sahihi na itakuwa ngumu kwenye mechi ya ushindani, ndiyo maana nakuwa naye karibu kumsisitiza na kila mchezaji namkumbusha hilo kujua jukumu lake na alifanye kwa usahihi.

"Kama unacheza winga, beki ama mshambuliaji, unapaswa ujue jukumu lako, lakini kuna wachezaji wengine hawajui majukumu yao, sisemi tu wachezaji wa Yanga, lakini ni wachezaji wengi naona sana kwenye ligi yetu wanacheza tu, hawajui majukumu yao, lakini kazi ya mwalimu ni kuwaelekeza na kuwarejesha kufahamu wanachopaswa kufanya," alisema.

Katika mazoezi ya Yanga yaliyodumu kwa masaa mawili na dakika 28, kuanzia saa 4:30 asubuhi hadi saa 7:10 mchana, kocha huyo aligawa vikosi vyake katika makundi mawili, la viungo na washambuliaji peke yao kama ilivyokuwa kwa mabeki, akiwasisitizia kufunga na kutengeneza nafasi. Wakati wote alikuwa karibu na kila mchezaji na kumfuata kumpa maelekezo pale alipokosea na kumwonyesha namna ya kufanya kwa usahihi.

BINGWA

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
12h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
16h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
17h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
17h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’