Yanga leo imeingia siku ya pili ya maandalizi yake kuelekea mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids Fc ambao utapigwa Jumapili Oktoba 27 kwenye uwanja wa CCM Kirumba
Baada ya kuichapa Mbao 1-0 juzi na jana kuifunga Pamba Fc mabao 2-1 kwenye mchezo wa kirafiki, kikosi cha Yanga kimeelekeza nguvu zake kwenye mchezo huo
Mkufunzi wa Yanga Mwinyi Zahera amesema wanafahamu mchezo hautakuwa mwepesi lakini ni lazima wapate ushindi nyumbani ili kuwa na nafasi ya kusonga mbele hatua ya makundi
"Ili tuwe na nafasi ya kusonga mbele lazima tushinde nyumbani. Hatukushinda nyumbani mchezo dhidi ya Zesco ndio maana tulitolewa, hatupaswi kurudia makosa," amesema
"Nimeiona Pyramids ni timu nzuri, lakini hawatutishi, tunajua ujanja wao hivyo tumejipanga kuwashangaza hapa Mwanza"
Yanga inafanya mazoezi yake kwenye uwanja wa CCM Kirumba
Pyramids Fc inatarajiwa kuwasili nchini leo wakitokea moja kwa moja kwao Misri kwa usafiri wa ndege binafsi
Klabu hiyo inamilikiwa na mabilionea wakubwa huko Misri