Kiungo fundi Feisal Salum amesema kutokana na maandalizi wanayoendelea kuyafanya jijini Mwanza, wana kila sababu ya kushinda mchezo wa kwanza wa mtoano kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids Fc
Keshokutwa Jumapili Otoba 27, Yanga itashuka kwenye uwanja wa CCM Kirumba kuwakabili waarabu hao kutoka Misri katika mchezo ambao Yanga wanahitaji zaidi matokeo ya ushindi
Fei Toto amesema wamepata nafasi ya kuifuatilia Pyramids kupitia mikanda ya video hivyo wanazo taarifa za kutosha kuhusu timu hiyo na wanafahamu jinsi watakavyo-wakabili ili kuweza kupata matokeo
"Hawa jamaa wana timu nzuri. Tumewafuatilia mechi zao mbalimbali kupitia mikanda ya video. Lakini nikwambie, tumejipanga, Jumapili tumedhamiria tutawafunga tu," amesema
cutFei Toto amekuwa 'injini' ya safu ya kiungo ya Yanga akishirikiana na Abdulaziz Makame na Papy Tshishimbi ambaye kwa siku za karibuni amekuwa akipewa majukumu ya ushambuliaji zaidi
Yanga imeendelea kujifua uwanja wa CCM Kirumba kujiandaa na mchezo huo
Jana uongozi wa Yanga ulihamisha timu Hotel waliyofikia awali na kuweka kambi kwenye Hotel bora zaidi yenye hadhi ya nyota tatu
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, amesema wameamua kuwahamisha wachezaji kwenda Hotel yenye hadhi ya juu zaidi ili kuongeza utulivu na umakini kwenye maandalizi yao
"Tumehamisha kambi ya wachezaji wetu, tumehamia katika Hoteli ya Victoria Palace iliyopo Capripoint Road, ni karibu kabisa na Ikulu, hoteli hiyo ni ya nyota tatu," amesema