Kocha Mkuu wa Pyramids Fc Sebastien Desabre amesema wamekuja nchini kuchuana na Yanga wakisaka matokeo yatakayowapa nafasi ya kutinga hatua ya makundi
Hata hivyo, Desabre kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Uganda ambayo ilishiriki michuano ya Afcon 2019 iliyofanyika Misri, amesema mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa timu zote
Desabre amesema anawafahamu baadhi ya nyota wa Yanga akiwataja nahodha Papy Tshishimbi na mshambuliaji Juma Balinya

"Nawafahamu baadhi kama yule nahodha mwenye rasta (Tshishimbi) na Balinya (Juma) ni wachezaji wazuri. Mchezo hautakuwa mwepesi lakini tumekuja kutafuta ushindi," alisema Desabre muda mfupi baada ya kutua jijini Mwanza Jana
Desabre anamfahamu vizuri Balinya kwa kuwa alifanya nae kazi wakati akiinoa timu ya Taifa ya Uganda
Kwa nyakati tofauti, Desabre alimjumuisha Balinya kwenye kikosi cha Uganda Cranes