Mkwassa afunguka mipango ya Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
10 Oct 2017
Mkwassa afunguka mipango ya Yanga
Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa ameweka wazi kuwa wanapanga kujiimarisha katika masuala ya utawala, usajili na fedha ili kuona timu yao inafanya vizuri katika ligi ya ndani na mashindano ya kimataifa.

Kwenye mahojiano na Mwanaspoti, Mkwassa amesisitiza kwamba hesabu za Yanga ni za mbali sana na wana vikao vya mara kwa mara kuangalia nini cha kufanya huku akiwataka wadau wa klabu kutokuwa na presha kabisa.

“Katika usajili kuna maeneo ambayo mwalimu amepanga kuyaimarisha hivyo tutampa sapoti kubwa. Nafasi ya mchezaji wa kigeni ni moja, ila tutasikiliza mapendekezo ya mwalimu,” alisema Mkwasa, ambaye amewahi pia kuinoa timu hiyo.

Alisema kwamba usajili wao wa dirisha dogo hauangalii majina bali aina ya watu ambao, wakiingia katika kikosi cha Jangwani watawapa pointi tatu ndani na nje ya nchi.

“Tumekuwa na majeruhi wengi sana na tunaangalia namna ya kuwasaidia wachezaji wetu warejee uwanjani kwa haraka, tunahitaji kuwa na timu nzuri.

“Katika masuala ya fedha bado tunatafuta udhamini mwingine. Yanga ni timu kubwa na ina matumizi makubwa ya fedha hivyo tunahitaji kupata hela zaidi. Tunazungumza na baadhi ya kampuni kuona kama wanaweza kutusaidia,” alisema.

Katika hatua nyingine Mkwassa amesema beki Fiston Kayembe ambaye amekuwa katika kikosi cha Yanga akifanya majaribio, atasajiliwa baada uongozi kupokea ripoti ya kocha George Lwandamina.

"Kocha akisema amekubali uwezo wake tutamsajili haraka tu. Tatizo ni kwamba tulikosa mechi za kutosha za kirafiki na ndiyo sababu tukasimama katika kumsaini, sasa tumeanza kupata mechi, nadhani kocha atatupatia ripoti yake punde," amesema Mkwasa.

Beki huyo wa kati ana uwezekano mkubwa wa kusajiliwa kwenye dirisha dogo la usajili katikati ya mwezi wa 11.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
33m ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
58m ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
12h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →