Pamoja na kujiunga na klabu ya Fanja Fc ya Oman, mshambuliaji wa zamani wa Yanga Amissi Tambwe amewatakia kila la kheri mabingwa hao wa kihistoria kwenye mchezo wao wa kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids Fc ambao utapigwa leo uwanja wa CCM Kirumba
"Nawatakia kila la kheri, Mungu awajaalie ushindi inshallah," aliandika Tambwe kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram
Naye mlinda lango Deogratius Munishi 'Dida' ameungana na Tambwe kuitakia kheri Yanga kwenye mchezo wa leo

"Kila la Kheri timu ya Wananchi..! Afe kipa Afe beki Ushindi Muhimu...! Taifa Lote lipo nyuma yenu Maana Nyinyi ndio Wawakilishi mlio baki katika Taifa hili ...! Mungu awabariki wote na mungu aibariki Tanzania"
Nyota hao walikuwa sehemu ya kikosi cha Yanga ambacho kilitwaa ubingwa wa ligi kuu kwa misimu mitatu mfululizo kati ya 2014 na 2017