GSM yaweka mezani Milioni 30 Yanga ikiitoa Pyramids

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Oct 2019
GSM yaweka mezani Milioni 30 Yanga ikiitoa Pyramids

Kampuni ya GSM ambao ni moja ya wadhamini wa klabu ya Yanga pia wakiwa wasambazaji wakuu wa jezi za klabu hiyo, leo wametoa ahadi ya kitita cha Tsh Milioni 30 kama Yanga itafanikiwa kutinga makundi

Ahadi hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, Mhandisi Hersi Said katika hafla ya kuwakabidhi wachezaji kitita cha Tsh Milioni 10 ahadi waliyotoa mechi dhidi ya Mbao Fc

Said amesema Milioni 30 iko mezani kwa ajili yao kama watapata matokeo dhidi ya Pyramids baada ya michezo yote miwili na kufanikiwa kutinga makundi

Ahadi hiyo inaongeza fedha ambazo wachezaji wa Yanga watapata kama watatinga makundi kufikia Milioni 130 baada ya hapo jana kocha Mwinyi Zahera kutoa ahadi ya Tsh Milioni 100

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji kwenye hafla hiyo, nahodha msaidizi wa Yanga Juma Abdul amewashukuru GSM kwa kuendelea kuwahamasisha

Amesema watahakikisha wanaendelea kufanya vizuri ambapo leo ameahidi wamejipanga kushinda kuanzia mabao mawili

Β 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’