Mashabiki wa Yanga wameendelea kuingia kwa wingi uwanja wa CCM Kirumba kuelekea mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids Fc ambao utaanza saa kumi Alasiri
Muitikio huo wa Wanayanga wa jijini Mwanza na wengine waliosafiri kutoka mikoani, ni jambo jema kwani timu itakuwa na sapoti ya kutosha
Shamrashamra za ushangiliaji zimeanza mapema mashabiki wakitakiwa kufanya hivyo kwa muda wote wa mchezo
Yanga haijawahi kufungwa mbele ya mashabiki wake jijini Mwanza katika mechi za Kimataifa, rekodi hiyo inapaswa kuendelezwa leo
ADVERTISE HERE