Kamati ya Utendaji ya klabu ya Yanga inatarajiwa kukutana kujadili mwenendo wa timu, imefahamika
Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya Yanga, zimebainisha kuwa kikao hicho kitafanyika leo
Kumekuwa na maoni, mapendekezo ya wadau baada ya kipigo cha mabao 2-1 kutoka Pyramids Fc jana
Aidha suala la kusuasua kwa timu msimu huu linatajwa kuwa moja ya ajenda ya kikao hicho
Mnyetishaji wetu amebainisha kuwa Kamati hiyo inaweza kuja na uamuzi wa kufanya mabadiliko benchi la ufundi
Hata hivyo kama uamuzi wa kuachana na kocha Mwinyi Zahera utaafikiwa, bado kutakuwa na changamoto ya kupata fedha za kuvunja mkataba wake
Wakati ikiweka mambo yake sawa, Yanga inaweza kumrejesha kocha wake wa zamani ambaye pia ni Mwanachama wake Hans van Pluijm
Aidha jina la Kim Poulsen kocha wa zamani wa timu za Taifa za vijana nalo linatajwa kupigiwa chapuo
Pengine uongozi wa Yanga umekisikia kilio cha wadau, ni suala la muda tu, tusubiri...