Kocha Mkuu wa Pyramids Sebastien Desabre ameeleza kuwa pamoja na kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa kwanza, bado wana kazi ya kufanya nyumbani ili kujihakikishia nafasi ya kutinga makundi
Aidha kocha huyo ameeleza kuvutiwa na viungo wawili wa Yanga Papy Tshishimbi na Feisal Salum 'Fei Toto'

Fei Toto alin'gara sehemu ya kiungo, akipiga mashuti kadhaa langoni kwa Pyramids wakati Tshishimbi ndiye aliyefunga bao pekee la Yanga kwenye mchezo huo
Kocha huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya Uganda, amesema mchezo wa kwanza ulikamilisha nusu ya mchezo na wanaelekea nyumbani kukamilisha nusu ya pili
"Ushindi tuliopata ni matokeo muhimu kuelekea mchezo wa marudiano nyumbani. Yanga ni timu nzuri, tutajipanga ili tupate matokeo mazuri nyumbani tuweze kuingia makundi"