Ligi Kuu msimu huu imekuwa na ushindani mkali na hivyo kuhitaji kujipanga ili kufanya vizuri
Pamoja na kuanza kwa kusuasua, Yanga bado ina nafasi ya kufanya vizuri hasa kutokana na matokeo ambayo timu nyingine zimeendelea kupata
Leo Simba imepoteza mchezo mkoani Shinyanga baada ya kuchapwa bao 1-0 na Mwadui Fc

Azam Fc moja ya timu zilizoanza msimu kwa kishindo, nayo mpaka sasa tayari imepoteza michezo miwili
Kufungwa kwa Simba na Azam Fc, kunatoa nafasi kwa Yanga kuweza kuzifikia timu hizo kama itaweza kushinda michezo yake baada ya kumaliza majukumu ya Kimataifa
Bado ni mapema sana kuzungumzia habari ya ubingwa lakini msimu huu lazima kieleweke...!
ADVERTISE HERE