Zahera katika mtihani Misri

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Nov 2019
Zahera katika mtihani Misri

Kesho Jumapili Yanga itashuka uwanja wa June 30 kuikabili Pyramids Fc ukiwa mchezo wa marudiano kombe la Shirikisho barani Afrika

Mchezo huo utakaopigwa saa tatu usiku, utakuwa wa pili baina ya timu hizo ambazo wiki iliyopita zilicheza jijini Mwanza na Pyramids Fc kushinda 2-1

Kikosi cha kocha Mwinyi Zahera kitaingia kwenye mchezo huo kikiwa na mahitaji ya ushindi wa angalau mabao mawili ili kuwa na nafasi ya kutinga hatua ya makundi

Lolote linaweza kutokea

Wakati mashabiki wakionyesha kukata tamaa na timu yao kutokana na matokeo ya mchezo wa kwanza, hali ni tofauti kwa wachezaji

Morali ya wachezaji iko juu, wamekuwa wakihamasishana huku wengine waitumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kuwahamasisha mashabiki

Hakuna shaka mchezo huo utakuwa mgumu kwa Yanga kwani Pyramids watakuwa wakicheza mbele ya mashabiki wao

Lakini kama wachezaji wa Yanga watakuwa na nidhamu, wanaweza kuwashangaza Pyramids

Zahera anafahamu kitakachotokea kama akifungwa

Hakuna ubishi, kibarua cha kocha Mwinyi Zahera kiko shakani kutokana na mwenendo wa Yanga msimu huu

Kipigo cha mchezo wa kwanza kiliwachochea mashabiki kushinikiza kocha huyo atimuliwe

Njia pekee ya kutuliza hali hiyo ni kwake kupata ushindi Misri

Kama Yanga itafungwa tena na Pyramids Fc, mashabiki hawatajali ukubwa wa timu hiyo, watakachotaka kuona ni kocha huyo kuonyeshwa mlango wa kutokea

Aidha imefahamika hata Kamati ya Utendaji ya Yanga ili-ahirisha kikao kilichokuwa kifanyike juzi kumjadili, kikao hicho kitafanyika baada ya mchezo huo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
11h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
15h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
16h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
16h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’