Pamoja na ushindi wa mabao 2-1 waliopata jijini Mwanza dhidi ya Yanga, Pyramids Fc inaonekana kupania mchezo wa marudiano ambao utapigwa kesho Jumapili huko Misri
Jana CEO wa klabu hiyo Mhandisi Mamdouh Eid alitimba mazoezini kushuhudia maandalizi ya kikosi chake pamoja na kuwahamisha wachezaji kuelekea mchezo dhidi ya Yanga


Pyramids Fc imeuchukulia mchezo huo kwa uzito mkubwa kwani kama wakivuka hatua hii na kutinga makundi, itakuwa mara yao ya kwanza katika historia yao
Hakika kutakuwa na kazi kubwa huko Misri, muhimu ni kuwatia moyo wachezaji wetu na kuwaombea ili waweze kupambana kwa dakika zote tisini kwani kwenye soka lolote linaweza kutokea
ADVERTISE HERE