Yanga yapania kuweka rekodi mpya Misri

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Nov 2019
Yanga yapania kuweka rekodi mpya Misri

Yanga leo ina kazi kubwa ya kupata ushindi mbele ya Pyramids Fc mchezo wa marudiano kombe la Shirikisho wakihitaji kupata ushindi angalau wa mabao 2-0 ili kutinga makundi

Matokeo ya mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Mwanza ndio yaliyoiweka Yanga kwenye wakati mgumu baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1

Katika mechi tisa ambazo Yanga imecheza Misri, matokeo mazuri yaliyopatikana ni sare dhidi ya Ismailia

Mechi nyingine Yanga ilipoteza dhidi ya miamba ya soka Al Ahly na Zamaleki ingawa mwaka 2014 nusura ipenye mbele ya Al Ahly baada ya kufungwa kwa changamoto ya mikwaju ya penati

Penati zilipigwa baada ya Yanga kushinda 1-0 nyumbani na Al Ahly kushinda 1-0 hapo Misri

Lakini katika mechi za hivi karibuni pamoja na kupoteza, Yanga imekuwa ikitoa ushindani mkali inapocheza Misri

Mchezo wa mwisho Yanga kupoteza Misri, ilifungwa 2-1 na Al Ahly katika mchezo ambao Al Ahly walikuwa na wakati mgumu kwelikweli

Hivyo kama Yanga itafanikiwa kuibuka na ushindi leo, itaanza ukurasa mpya dhidi ya timu za Misri

Mafanikio ya Yanga kwenye mchezo wa leo, yatatokana na utulivu wa wachezaji

Dakika za mwanzo ni muhimu sana kwa Yanga kuhakikisha hawaruhusu bao la mapema

Kwani moja ya mbinu zinazotumiwa na timu za Misri ni kuwaweka katika presha kubwa wapinzani wao kwenye dakika za mwanzoni ili kupata mabao ya mapema

Lakini kama Yanga itafanikiwa kuwazuia Pyramids kwa dakika zote 45 za kipindi cha kwanza, uwezekano wa kuwafunga kwenye kipindi cha pili ni mkubwa

Takwimu zinaonyesha Pyramids imekuwa ikiruhusu mabao mengi kwenye kipindi cha pili hasa dakika 15 za mwisho

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’