Beki Ally Ally ameendelea kudhihirisha ubora wake baada ya jana kuonyesha kiwango cha hali ya juu kwenye mchezo dhidi ya Pyramids Fc nchini Misri
Ally aliyecheza kwa dakika 70, alionyesha utulivu wa hali ya juu kwenye mchezo huo huku akiwa bora katika kucheza mipira ya juu
Pengine majeraha aliyopata kwenye dakika ya 70 na kulazimika kutoka, yalichangia safu ya ulinzi ya Yanga kupoteana na kuruhusu mabao mawili kwenye dakika 10 za mwisho
Ally alishikiana vyema na Lamine Moro ambaye naye hakumaliza mchezo baada ya kutonesha majeraha ya paja
Lamine alilazimika kucheza mchezo huo huku ukiwa na majeraha
Alishindwa kuendelea na mchezo kwenye dakika ya 85, wakati huo Yanga ikiwa imemaliza 'sub' hivyo kulazimika kucheza na wachezaji 10
ADVERTISE HERE