Tulikuwa bora zaidi mechi ya Pyramids - Zahera

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Nov 2019
Tulikuwa bora zaidi mechi ya Pyramids - Zahera

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema pamoja na timu yake kufungwa mabao 3-0 na Pyramids Fc katika mchezo wa kombe la Shirikisho hapo jana, amewapongeza vijana wake kwa kuonyesha kandanda safi

Zahera amesema wachezaji jana walicheza vizuri kuliko mechi zote walizocheza msimu huu

"Nawapongeza wachezaji wangu, nafikiri jana tulionyesha mchezo bora kuliko mechi zote tulizocheza katika michuano ya Kimataifa msimu huu," amesema

Aidha Zahera ameongeza kuwa kocha wa Pyramids Fc alikiri kuwa mchezo wa jana ulikuwa mgumu kuliko mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Mwanza

"Kocha wao anasema baada ya kuwapa wakati mgumu kwenye mchezo wa kwanza, walidhani labda ni sababu ya uwanja"

"Lakini jana wameshangaa kuona mchezo ulikuwa mgumu zaidi licha ya kuchezwa katika uwanja wao"

Katika mchezo huo Yanga ilipoteza umakini kwenye dakika 10 za mwisho na kujikuta ikiruhusu mabao mawili

Aidha ni wakati huo ambao walinzi Ally Ally na Lamine Moro walipata majeraha hali iliyomlazimu Papy Tshishimbi kurudi kucheza namba tano

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’