Nahodha msaidizi wa Yanga Thabani Kamusoko anasumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu hivyo huenda asisafiri na kikosi cha Yanga kinachoelekea kanda ya ziwa kwa ajili ya michezo miwili dhidi ya Kagera Sugar na Stand United.
Aidha Donald Ngoma hali yake imeendelea kuimarika na huenda akajumuishwa katika kikosi cha Yanga kitakachosafiri kesho Alhamisi kwenda mkoani Bukoba.
Mlinda lango Ramadhani Kabwili na winga Saidi Mussa wameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa chini ya umri wa miaka 20 hivyo hawatakuwemo katika safari hiyo ya kanda ya ziwa.
Ikumbukwe baada ya michezo miwili ya kanda ya ziwa, Yanga itarejea jijini Dar es salaam kuumana na Simba Oktoba 28.
Nadhani ni jambo jema kumuacha Kamusoko apone kabisa ili awe tayari kutumika kwenye mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

ADVERTISE HERE